Breaking News

VIJANA WASHAURIWA KUACHA MIHEMKO NA KUILINDA AMANI



Wananchi wa Mkoa wa Dar Es salaam wameeleza kuwa mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali nchini pamoja na ukosefu wa huduma na bidhaa muhimu kulikotokana na ghasia na vurugu za Oktoba 29, 2025 kumewaathiri kiuchumi, wakiwataka Vijana kuacha mihemko na kutokubali kurubuniwa katika kuharibu amani na utulivu uliopo nchini.

Wananchi hao kwa nyakati tofauti wakizungumza na waandishi wa habari akiwemo Bw. Rahim Hassan Bakari, Mfanyabiashara wa soko la Kariakoo amesema kwa siku sita za ghasia hizo na zuio la kutofanya biashara kwa saa 24 kama walivyozoea limesababisha mfumuko huo ikiwemo katika bidhaa za vyakula ambapo nyanya moja kwasasa inauzwa shilingi 1, 000 kutoka Shilingi 100 huku Mchele ukiuzwa Kilo moja Shilingi 4,000 badala ya 2500.

"Vijana wenzangu nawashauri tuache mihemko, kilichotokea juzi kilikuwa mihemko tu kwasababu leo ukimuuliza aliyeandamana kwamba kwanini aliandamana atakuambia hana majibu. Mimi niombe tu kuwa tuache mihemko na kama tuna madai mbalimbali tufuate njia sahihi za kushughulikia changamoto zetu." Amesisitiza Bw. Bakari.

Kwa upande wake Bi. Faizat Peter, Mkazi wa Mbagala Jijini Dar Es Salaam ameeleza namna ambavyo maandamano hayo yamemuathiri kiuchumi na kijamii, akitoa wito wa amani nchini Tanzania na Watanzania wote kufanya tafakuri na kujifunza kutokana na athari zilizojitokeza Oktoba 29 kutokana na vurugu na ghasia zilizotokea Mkoani Dar Es Salaam, Mwanza, Arusha, Songwe na Mbeya.




from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/c4xqpPJ

No comments