Breaking News

KIVUMBI TAMASHA LA AMANI NA MAENDELEO KISHAPU


Na Sumai Salum- Kishapu

Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga imewaka moto wa michezo kufuatia kuendelea kwa Tamasha la Amani na Maendeleo linalofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Buduhe.


Tamasha hilo lililoanza rasmi Februari 23, 2026 linatarajiwa kuhitimishwa Februari 28, 2026, likiwa limekusanya mamia ya washiriki na mashabiki kutoka maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.


Katika mchezo wa dakika 90 uliopigwa leo, timu ya Kishapu Veteran imeonyesha ubabe kwa kuichapa Mafundi FC mabao 4-0, ushindi uliotikisa tamasha na kuacha mashabiki wakishangilia kwa nderemo na vifijo huku Mafundi FC, msumeno wao leo haukukata kama ilivyotarajiwa, mshambuliaji Benjamini akiipa timu yake bao 1 la kufutia machozi.



Wafungaji wa Kishapu Veteran ni Lupatiko (magoli 2), Santos (goli 1) na Sheby (goli 1).



Ushindi huo umeifanya Kishapu Veteran kuvuna pointi muhimu na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania taji la tamasha hilo.



Tamasha hilo limeendelea pia kushuhudia michezo mingine yenye ushindani mkali huku mpira wa wavu wakishindana Kishapu Sekondari dhidi ya Veta Kishapu na Kishapu wakiibuka na 2 kwa nunge (0) .



Aidha kwa upande wa mpira wa pete Isoso Sekondari 6 huku Mwataga Sekondari wakipata 7 na mechi kati ya Kishapu Sekondari na Veta Kishapu, Kishapu Sekondari wameibuka na 6 huku Veta wakipata 3.



Ushindani katika michezo hiyo umeonyesha vipaji vya hali ya juu kwa vijana, huku shule na taasisi zikionesha maandalizi makubwa.


Mbali na michezo, tamasha hilo limepambwa na burudani za ngoma za asili, ikiwemo kikundi maarufu cha Chapa Kazi Mwabusiga, kilichotoa burudani ya aina yake.


Sherehe za tamasha hilo zitafikia kilele kwa mkesha wa kukata na shoka utakaofanyika kwa siku mbili mfululizo — Ijumaa na Jumamosi — ukitarajiwa kuvuta umati mkubwa wa wananchi kusherehekea amani, mshikamano na maendeleo kupitia michezo.



Tamasha la Amani na Maendeleo Kishapu linaendelea kuthibitisha kuwa michezo ni daraja la umoja, furaha na maendeleo ya jamii. 🏅




















































































































































from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/lzrhTQF

No comments