CHALAMILA AFICHUA MADUDU ARDHI DAR, "RUDISHENI ARDHI YA WATU NDANI YA WIKI MOJA"
-RC Chalamila awapa siku 7 waliopora ardhi na mali za wananchi kuzirejesha; asema msamaha upo kwa watakaojisalimisha wenyewe.
-Kigamboni na Ilala yatajwa kuongoza kwa dhuluma za viwanja na mikataba kandamizi ya mikopo.
- RC aanika madudu; adai kuna wananchi wamelipa hadi Sh. Milioni 100 lakini hawajapewa magari yao.
Ziara ya Machi 9: Mkuu wa Mkoa kutembelea maeneo yaliyoathirika kusikiliza kero; atoa namba maalum (0733 206 952) kwa wahanga kutoa taarifa.
Zaidi ya maeneo 16 tayari yamerudishwa kwa siri baada ya shinikizo la Serikali kuanza kufanya kazi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewasha moto dhidi ya matapeli wa ardhi na mali jijini hapa, akitoa agizo la mwisho la wiki moja kwa wote waliodhulumu wananchi kurejesha mali hizo kabla ya "mkono wa dola" haujawafikia.
Akizungumza na wanahabari leo, RC Chalamila amesema Serikali imechoshwa na malalamiko ya wanyonge wanaopoteza viwanja na nyumba kupitia mikataba ya hila na utapeli wa kimfumo. Amesema kuwa operesheni hiyo haitaishia kwenye ardhi pekee, bali itafika hadi kwenye biashara za magari (showrooms) ambako baadhi ya wateja wameibiwa mamilioni ya fedha bila kupewa magari yao.
"Kuna watu wamesainisha wananchi mikataba ya mauzo ya nyumba badala ya mikataba ya mikopo. Huku ni kuumiza watu. Nawapa wiki moja, rudisheni mali za watu wenyewe mtoe usumbufu," amesisitiza Chalamila.
Aidha, RC huyo ameweka wazi kuwa kuanzia Machi 9, 2026, ataanza ziara rasmi kwenye maeneo yenye migogoro mikubwa ili kukutana na wahanga uso kwa uso. Amewahimiza wananchi waliodhulumiwa kutumia namba ya simu 0733 206 952 kuwasilisha ushahidi wao ili hatua zichukuliwe mara moja.
.jpeg)
No comments