Waziri Kitila: Dira 2050 kuanza rasmi Julai mosi, miradi ya Trilioni 120 yapewa kipaumbele.

Tume ya Taifa ya Mipango imeidhinisha rasmi miongozo minne itakayotumika kusimamia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2050, inayotarajiwa kuanza rasmi Julai Mosi mwaka huu.

Akizungumza Ikulu jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Profesa Kitila Mkumbo, alisema kuwa taifa linaanza safari hii likiwa na nyenzo zote muhimu tofauti na dira iliyopita ya mwaka 2025 ambayo ilianza ikiwa na nyenzo moja tu. 

Miongozo hiyo iliyopitishwa ni pamoja na Mwongozo wa Kitaifa wa Mipango utakaolazimisha wizara na mamlaka za mitaa kuandaa mipango yao, Mwongozo wa Kitaifa wa Uidhinishaji wa Miradi ya Maendeleo ambao unaipa tume mamlaka ya kuchuja miradi kabla ya malipo, Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo kwa ajili ya kutoa viashiria vya upimaji, pamoja na Mkakati wa Mawasiliano wa miaka mitano wa Dira 2050 (2026/27-2030/31) unaobainisha jinsi vyombo vya habari vitakavyoshirikishwa kutoa taarifa za maendeleo.

Viashiria Vya Mageuzi na Maeneo ya Kipaumbele

Mbali na miongozo hiyo, serikali imeidhinisha maeneo makuu matatu ya kimkakati yanayohitaji mageuzi makubwa yenye jumla ya viashiria vya upimaji 142.

Maeneo hayo ni mageuzi katika mifumo ya utawala na utumishi wa umma yenye viashiria 13, mageuzi katika uwekezaji na uzalishaji yenye viashiria 53, pamoja na mageuzi katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi na mazingira yenye viashiria 76. Sambamba na hayo, zimetajwa sekta za kipaumbele 12 zenye jumla ya viashiria 206, zikiwemo sekta ya Kilimo, Ujenzi, Madini na Nishati, Utalii, Ubunifu na Maudhui ya Kidijiti, Milki, Ardhi na Maendeleo ya Miji, Biashara na Uwekezaji, Elimu, Hifadhi ya Jamii na Kazi, Uchumi wa Buluu, pamoja na Sayansi, Teknolojia na Uchumi vya Kidigiti. 

Profesa Kitila alisisitiza kuwa watendaji wote watapimwa kwa kuangalia matokeo halisi na sio michakato au shughuli tu, ili kuhakikisha ufanisi wa hali ya juu.

Nafasi ya Sekta ya Michezo na Sanaa Kiuchumi

Katika dira hiyo mpya, sekta ya michezo na sanaa imetambuliwa rasmi kama nguzo muhimu ya kiuchumi na kijamii nchini, ambapo imepewa viashiria tisa vya kupima ukuaji na mafanikio yake. 

Serikali inapanga kutumia viashiria hivyo kupima kiasi cha fedha kinachozalishwa moja kwa moja na sekta ya michezo, ubunifu, burudani na sanaa, pamoja na idadi ya vijana walioajiriwa rasmi kama wanamichezo, waigizaji, wanamuziki, na wabunifu wa maudhui ya kidijiti. 

Aidha, dira hiyo itafuatilia ongezeko la mapato ya mauzo ya kazi za sanaa nje ya nchi, utalii wa kitamaduni, maendeleo ya vipaji kupitia ujenzi wa vituo maalum vya ukuzaji vipaji kwa watoto na vijana, pamoja na upatikanaji na ubora wa viwanja vya kisasa vya michezo and kumbi za sanaa nchi nzima.

 Pia, itapima mafanikio ya timu za taifa na wasanii katika mashindano ya kikanda na kimataifa, ikilenga kujenga maadili mema na uzalendo kwa vijana.

Mageuzi ya Kimfumo na Mapungufu ya Dira ya 2025

Tathmini ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 imeonesha kuwa pamoja na kuwepo kwa ukuaji wa uchumi, mafanikio hayo hayakuweza kupunguza umaskini kwa kiwango kilichotarajiwa wala kuzalisha ajira za kutosha zenye staha.

Profesa Kitila alibainisha kuwa sekta zilizoongoza ukuaji huo kama madini na utalii hazikugusa wananchi wengi moja kwa moja, na taifa lilikwama katika kuhamisha nguvu kazi kutoka kilimo kwenda viwandani. Kutokana na mafunzo hayo, Dira ya 2050 imejikita katika nguzo nne kuu ambazo ni ustawi jumuishi, uzalishaji wa ajira, haki na kujitegemea.

Katika mageuzi ya kimfumo, serikali imepanga kukamilisha mchakato wa Katiba Mpya pale ulipoishia kwa kuwa sasa umeingizwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kupunguza urasimu wa kiofisi, kuboresha uhusiano na sekta binafsi ili isionekane kama mshindani, na kuimarisha uwajibikaji kupitia uhuru wa vyombo vya habari.

Ukuaji wa Uwekezaji na Hatua za TISEZA

Mamlaka ya Maeneo Maalumu ya Uwekezaji Tanzania (TISEZA) imeeleza kuwa maboresho ya mazingira ya biashara, mageuzi ya mifumo ya uwekezaji, na diplomasia ya uchumi inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan vimeifanya Tanzania kuongoza katika kuvutia uwekezaji Afrika Mashariki. 

Mkurugenzi wa TISEZA, Gilead Teri, alieleza kuwa marekebisho ya Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 2022 na uboreshaji wa sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na binafsi (PPP) ya mwaka 2023 vimeongeza usalama wa mitaji. 

Hatua ya mwaka 2025 ya kuunganisha mamlaka mbalimbali na kuunda kituo kimoja cha TISEZA imesaidia kukuza uwekezaji kutoka Dola za Marekani bilioni tatu mwaka 2021 hadi kufikia Dola bilioni 12 mwaka 2025, huku zaidi ya ajira 500,000 zikitengenezwa. Profesa Kitila aliongeza kuwa sifa kuu nne zinazoibeba nchi ni jiografia yake ya kimkakati yenye bahari, rasilimali adimu, nguvu kazi kubwa ya watu, pamoja na amani na utulivu wa zaidi ya miaka 60.

Miradi ya Kimkakati ya Shilingi Trilioni 120

Ili kujenga msingi imara wa kufikia uchumi wa Dola za Marekani trilioni moja ifikapo mwaka 2050, serikali imetoa agizo la kukamilishwa kwa haraka ndani ya mwaka mmoja majadiliano yote ya kisheria na wawekezaji kuhusu miradi minne mikubwa ya kimkakati yenye thamani ya jumla ya Shilingi trilioni 120 (sawa na Dola bilioni 47.9).

 Miradi hiyo ni pamoja na mradi unganishi wa chuma cha Liganga na Makaa ya Mawe ya Mchuchuma wa Shilingi trilioni tisa, mradi wa magadi soda wa Engaruka wa Dola milioni 400, mradi wa Nickel wa Kabanga na kiwanda cha usafishaji cha Kahama wa Dola bilioni 2.5, pamoja na mradi mkubwa wa kuchakata gesi asilia kuwa kimiminika (LNG) wa Dola bilioni 42.

Profesa Kitila alifafanua kuwa mazungumzo ya msingi na ya mgawanyo wa kibiashara yamebaki upande wa mifumo ya kisheria kwa sababu baadhi ya wawekezaji wanapendekeza masharti ya kimataifa na uwepo wa sheria maalum ya mradi, jambo ambalo ni geni nchini.

 Hata hivyo, serikali ipo makini kulinda maslahi ya taifa ili kuepuka hasara na migogoro ya kisheria ya kimataifa hapo baadaye, huku ikihakikisha sehemu ya futi za ujazo trilioni 57 za akiba ya gesi asilia inatumiwa ndani ya nchi kwa manufaa ya wananchi

Post a Comment

Previous Post Next Post