Vijana wengi hupenda kujaribu vitu vipya, na hilo linaonekana pia kwenye mazungumzo yanayoendelea kuhusu ORIJIN wiki moja baada ya kuzinduliwa nchini. Kinywaji hicho kimeendelea kuvutia wanaotafuta ladha tofauti na walizozoea.
Tofauti kati ya ORIJIN Bitters na ORIJIN Mixed (RTD) ni miongoni mwa mambo yanayoulizwa na kujadiliwa na watumiaji. Wakati wengine wakilinganisha aina hizo mbili, wengine wanavutiwa zaidi na mchanganyiko wake uliotokana na herbs, roots na fruits za Kiafrika.
Wiki moja baada ya kuzinduliwa rasmi nchini, ORIJIN imeendelea kuwa miongoni mwa bidhaa zinazozungumzwa na watu wa makundi mbalimbali. Kilichoonekana zaidi si tu watu kuionja, bali namna kila mmoja anavyokuwa na maoni yake kuhusu ladha yake.
Wapo wanaosema ladha yake imewarudisha kwenye kumbukumbu za vinywaji vya asili walivyovifahamu zamani, huku wengine wakieleza kuwa ni ladha mpya ambayo hawajawahi kuikuta kwenye bidhaa nyingine walizowahi kutumia. Tofauti hizo ndizo zimeendelea kufanya mazungumzo yasikome.
Kadri watu wanavyoendelea kuifahamu, ORIJIN inaonekana kujijengea nafasi yake sokoni kupitia maoni yanayotolewa na walaji wenyewe, jambo linaloifanya ibaki kwenye mjadala hata baada ya uzinduzi kupita.
Kwa sasa, ORIJIN Mixed (RTD) inapatikana kwa Sh3,000, huku ORIJIN Bitters ikipatikana katika ukubwa tofauti kwa Sh5,000 na Sh15,000, hivyo kuwapa watumiaji uhuru wa kuchagua kulingana na bajeti na mapendeleo yao.
