RAIS DKT. SAMIA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA TEC


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 10 Agosti, 2026, amekutana na kufanya mazungumzo na Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania kupitia Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference - TEC), Ikulu ya Chamwino, mkoani Dodoma. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu,Bakari S. Machumu, mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Serikali na TEC na kujadili masuala mbalimbali ya kitaifa yanayoigusa jamii, yakiwemo ya kisiasa, imani na maendeleo, pamoja na kuimarisha amani, mshikamano na kujenga mustakabali mwema wa Taifa. 

Aidha, mazungumzo hayo yaligusia umuhimu wa nafasi ya madhehebu na Viongozi wa Dini katika kulea jamii yenye maadili mema, uwajibikaji na mshikamano, ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika ustawi na maendeleo endelevu ya Taifa. 

Mheshimiwa Rais aliwashukuru Maaskofu hao kwa kuona umuhimu wa kukutana na kujadiliana naye masuala yenye tija kwa Taifa na kuwahakikishia dhamira yake ya kuendeleza utamaduni wa kushauriana na kushirikisha Viongozi wa Dini na makundi mbalimbali katika jamii kuhusu masuala muhimu ya kitaifa kila inapohitajika.







from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/qOLAtmo

Post a Comment

Previous Post Next Post