Mwenyekiti wa Umoja wa "Ishi na Watu Kijamii Kishapu" John Maliganya(Kulia) akimkabidhi tisheti ya kikundi hicho Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa mkutano mkuu wa kikundi hicho Mhe. Peter Masindi (kushoto) Septemba 26, 2026 ukumbi wa Storm Palace Hotel
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, akizungumza leo Septemba 26, 2026, akiwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kikundi cha Ishi na Watu Kijamii Kishapu uliofanyika ukumbi wa Storm Palace Hotel
Na Sumai Salum-Kishapu
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amewapongeza wanachama wa Umoja wa Ishi na Watu Kijamii Kishapu kwa kuendeleza umoja na ushirikiano, akieleza kuwa mshikamano ni muhimu katika kukabiliana na umaskini, maradhi na ujinga.
Akizungumza Leo Septemba 26, 2026, akiwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kikundi hicho uliofanyika ukumbi wa Storm Palace Hotel, ameupongeza Umoja wa "Ishi na Watu Kijamii Kishapu" kwa kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na utamaduni wa kusaidiana, akisema hatua hiyo ni muhimu katika kujenga jamii yenye nguvu na yenye kujali ustawi wa kila mmoja.
"Kundi hili nimeona linainarika siku Hadi siku na kujiwekea Mipango mbalimbali kupitia mtandao wa "Whatsap" niwasihi jukwaa hilo lisitumike kumkashifu mtu au kiongozi yeyote achaneni na mijadala isiyo na tija katika makundi ya mitandao ya kijamii, badala yake mtumie majukwaa hayo kujadili masuala yenye manufaa, kupeana fursa na kujenga uchumi" amesisitiza Masindi.
Amesema Serikali inathamini jitihada za wananchi kuungana na kusaidiana katika kutatua changamoto mbalimbali, hivyo amewataka wanachama kuendelea kuulinda umoja huo, kuheshimiana na kutumia fursa zilizopo, ikiwemo mikopo ya Serikali kupitia Halmashauri, ili kuendeleza shughuli za kiuchumi na kujikwamua kimaisha.
Masindi amewapongeza wanachama kwa moyo wa kujitolea na kusaidiana akisema hatua ya kutumia rasilimali zao kuwasaidia wenzao wakati wa matatizo inaonesha umoja huo una nafasi kubwa katika kujenga jamii yenye mshikamano na utu.
Mwenyekiti wa Umoja wa "Ishi na Watu Kijamii Kishapu" John Maliganya akizungumza kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kikundi hicho uliofanyika Septemba 26, 2026 ukumbi wa Storm Palace Hotel
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa "Ishi na Watu Kijamii Kishapu" John Maliganya, amesema umoja huo umejengwa katika misingi ya upendo, mshikamano na kusaidiana wakati wa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanachama.
Amesema kikundi hicho kina jumla ya wanachama 383, ambao wameendelea kushirikiana kwa kuchangia na kusaidiana pale mwanachama au jamii inapokumbwa na matatizo, ambapo hadi sasa wamefanikiwa kutoa zaidi ya Shilingi milioni 15 kwa ajili ya kuwasaidia watu waliokumbwa na changamoto mbalimbali.
"Mkuu wetu wa Wilaya, Umoja huu unalenga kujenga mshikamano miongoni mwa wanachama, kusaidiana na kuimarisha mahusiano, pia niwaombe wanachama wenzangu tuendelee kushirikiana na kusaidiana wakati wa changamoto" amesisitiza Maliganya.
Maliganya amewataka wanachama kuendelea kuutunza umoja huo, kuheshimiana na kushirikiana bila kujali tofauti zao, akisisitiza kuwa nguvu ya kikundi hicho ipo katika umoja na moyo wa kila mmoja kuwa tayari kumsaidia mwenzake.
Pia amewashukuru viongozi wa Serikali kwa kutambua na kuunga mkono juhudi za kikundi hicho, akisema ushirikiano kati ya Serikali na wananchi ni muhimu katika kuimarisha maendeleo na ustawi wa jamii.
Diwani wa Kata ya Kishapu wilayani Kishapu mkoani Shinyanga na mmiliki wa Hoteli ya Storm Palace, Mhe. Joel Ndettoson akizungumza leo Septemba 26, 2026, kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kikundi cha Ishi na Watu Kijamii Kishapu uliofanyika ukumbi wa Storm Palace Hotel
Diwani wa Kata ya Kishapu, Mhe. Joel Ndettoson amepongeza umoja na mshikamano wa wanachama hao, akisema ushirikiano wao ni msingi wa kusaidiana na kuinua maisha ya jamii.
Mmoja wa wanachama wa umoja huo Mary Mgimwa, amesema kikundi cha Ishi na watu kijamii Kishapu umefanyika msaada na baraka kwa wanachama kwani wamekuwa wakikimbiliana na kufarijiana wakati wa misiba pindi mtu akifikwa na janga hata kama hana kitu anapata mwanzo mpya wenye matumaini.
Ishi na watu Kijamii Kishapu ni kikundi kilichokusaya watu wanaoishi Kishapu na ambao wamehamia maeneo mengine nje ya Kishapu lakini bado wanaona kuna thamani kubwa kuendelea kuwa wanachama wa kikundi hicho jambo walilolithibitisha kwa kuacha shughuli na familia zao kutokea sehemu mbalimbali za Tanzania na kuja Kishapu kushiriki mkutano mkuu wa mwaka 2026.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, akizungumza leo Septemba 26, 2026, akiwa mgeni rasmi kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa kikundi cha Ishi na Watu Kijamii Kishapu uliofanyika ukumbi wa Storm Palace Hotel
Katibu Msaidizi wa kikundi cha Ishi na watu Kijamii Kishapu Ester Paschal akisona risala kwa mgeni rasmi ya kikundi hicho
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM Mkoa wa Shinyanga Benard Werema akifuatilia mkutano huo kwa makini
Mwanachama wa Kikundi cha Ishi na Watu Kijamii Kishapu Mary Mgimwa
Mwenyekiti wa Umoja wa "Ishi na Watu Kijamii Kishapu" John Maliganya(Kushoto) akiteta jambo na mgeni rasmi wa mkutano mkuu wa kikundi hicho ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi (kulia) Septemba 26, 2026 ukumbi wa Storm Palace Hotel
Tazama Picha za Matukio mbalimbali hapa chini
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/FZEc5K1
Tags
News
