KAIMU
Mkurugenzi wa Mfuko wa Bodi ya Bima ya Amana, Bw. Richard Malisa, ameshauri
kuwa mwananchi kabla hajafungua akaunti kwenye benki fulani ni bora ajiridhishe kuhusu uwezo wa benki hiyo.
Bw.
Malisa aliyasema hayo leo Desemba 12, 2018 wakati akiwasilisha mada iliyoelezea
kazi za Bodi ya Bima ya Amana na Ufilisi wa mabenki na taasisi za fedha:
mafanikio na changamoto, kwa waandishi wa habari za uchumi na fedha kwenye ukumbi
wa Benki Kuu ya Tanzania tawi la Dodoma.
“Usiweke
fedha kwenye benki ambayo huna uhakika nayo, kwa kufanya hivyo utasaidia
kulinda mfuko ili uwe na uwezo wa kuhudumia wananchi (wateja), lakinin pia usalama wa fedha zako.” Alisema Bw.
Malisa.
Alisema,
kwa mujibu wa sheria ya BoT, Benki inapoanzishwa lazima iwe na mtaji wa kima cha
chini cha shilingi bilioni 15, na benki hiyo hairuhusiwi kumkopesha mtu mmoja
au kampuni moja asilimia 20 ya mtaji wake.
Alisema,
kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kiundeshaji, benki inaweza kufa na inapotokea benki imekufa, Bodi ya Bima ya
Amana huchukua jukumu la kuwalipa kiasi cha fedha wateja wa benki hiyo." Alisema Bw. Malisa na kuongeza"Mteja wa benki iliyofungwa (kufa) aliyeweka amana za zaidi ya shilingi milioni 1.5 atalipwa shilingi milioni 1.5, na mteja aliyeweka amana chini ya kiasi hicho cha fedha atalipwa fedha zake zote." Alifafanua.
KAIMU
Mkurugenzi wa Mfuko wa Bodi ya Bima ya Amana, Bw. Richard Malisa, akiwasilisha mada kuhusu kazi za Bodi ya Bima ya Amana na Ufilisi wa mabenki na taasisi za fedha:
mafanikio na changamoto.
KAIMU
Mkurugenzi wa Mfuko wa Bodi ya Bima ya Amana, Bw. Richard Malisa, akiwasilisha mada kuhusu kazi za Bodi ya Bima ya Amana na Ufilisi wa mabenki na taasisi za fedha:
mafanikio na changamoto.
Kutoka kushoto, Meneja wa Uhusiano wa Umma na Itifaki BoT, Bi. Zalia Mbeo, (wakwanza kushoto), Meneja wa BoT kanda ya Kati anayeshughulikia masuala ya uchumi na tafiti, Dkt. Zegezege E.Mpemba, (watatu kulia), Dkt. Camillus Alphonce Kombe, Meneja wa Uchumi na Takwimu BoT Dodoma, (wapili kulia) na Mshauri wa BoT tawi la Dodoma Bw. Stanslaus T. Mrema, wakijadiliana jambo.
KAIMU
Mkurugenzi wa Mfuko wa Bodi ya Bima ya Amana, Bw. Richard Malisa, akiwasilisha mada kuhusu kazi za Bodi ya Bima ya Amana na Ufilisi wa mabenki na taasisi za fedha:
mafanikio na changamoto.
Bw. Said Mwinshehe kutoka Michuzi Blog.
Sehemu ya washiriki.
Baadhi ya maofisa wa BoT.












