NA MWANDISHI WETU
MFUKO wa hifadhi ya Jamii kwa sekta binafsi nchini(NSSF),imekuwa ya kwanza kuanza kutekeleza agizo la Rais Dk John Magufuli,ya kutumia mfumo wa zamani wa kikokotoo katika malipo ya wastaafu nchini
Rais Dk. Magufuli katika mkutano wake na viongozi wa vyama vya vyafanyakazi, Mamlaka ya usimamizi na udhibiti wa sekta ya Hifadhi ya jamii, watendaji wakuu wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Mfuko,alieleza kuwa mashirika ya hifadhi ya jamii yatumie mifumo ya zamani kuwalipa wastaafu kwa kipindi cha mpito mpaka mwaka 2023 baada ya makundi na taasisi mbali mbali kulalamikia kikokotoo kipya kilichotokana na mifuko kuunganishwa
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar esSalaam,Meneja Kiongozi wa matekelezo wa NSSF,Cosmas Sasi, alisema wanaendelea kupokea na kuhakiki madai mbali mbali kutoka kwa wanachama ambao ajira zao zimekoma na ambao walikuwa kwenye ajira za muda maalumu kwenye sekta mbali mbali kama vile madini, viwanda, ujenzi na kilimo.
“Madai yote yanayothibitishwa kuwa ni halali baada ya kuhakikiwa, mwanachama atalipwa mafao yake na kwa sasa tunaendelea kulipa mafao kwa wanachama wetu”alisema Sasi
Alisema kwa kwa upande wa mafao ya uzeeni takribani shilingi bilioni 5 zimekuwa zinalipwa kila mwezi kwa wastaafu wao kuanzia julai 2018. Kwa pensheni ya mwezi Desemba, 2018 kiasi cha shilingi Bilioni 4.83i kimeshalipwa kwa wastaafu 18,631 waliokuwepo kwenye daftari Ia wastaafu.
Aliongeza kuwa kwa upande wa malimbikizo ya Mafao hadi kufikia julai 2018 jumla ya shillingi bilioni 108 zilikuwa zinadaiwa kwenye Shirika, ambapo kiasi cha shilingi bilioni 85 kimelipwa kwa wanachama waliokuwa na madai mbali mbali baada ya uhakiki kukamilika na kiasi kilichobaki cha shilingi bilioni 23 kitalipwa baada ya uhakiki unaondelea kukamilika.
Kwa upande wake, Meneja Kiongozi Uhusiano na Elimu kwa Uma (Lulu Mengele alisema Mfuko ulianza zoezi Ia kuhakiki wastaafu wake kuanzia Disemba 1mwaka jana na zoezi hilo linaendelea kwenye ofisi mbali mbali za NSSF zilizoko mikoa yote ya Tanzania Bara.
Aliwataka wastaafu ambao hawajajitokeza kuhakiki, wafike kwenye ofisi zao 65 zilizoko katika maeneo mbali mbali katika mikoa yote Tanzania bara kwa upande wa wastaafu wanaoishi Zanzibar,alisema watahakikiwa kwenye ofisi za ZSSF.
“Wastaafu wanatakiwa kuwa na nyaraka zifuatazo picha, kitambulisho cha Taifa au cha mpiga kura pamoja na kadi ya benki. Malipo ya pensheni kwa wastaafu ambao hawatahakikiwa yatasitishwa mwishoni mwa mwezi wa Januari 2019.Malipo ya wastaafu yatafanyika moja kwa moja kwenye akaunti za wastaafu ili kumrahisishia mstaafu kupata malipo yake ya pensheni kwa haraka na bila usumbufu,zoezi Ia uhakiki litakuwa endelevu ili kuboresha taarifa zi|izokuwepo kwenye daftari la wastaafu “alisema Mengele na kuongeza
“Shirika linasisitiza kwa wafanyakazi na maofisa utumishi kuhakikisha madai yanayoletwa kwenye Mfuko ni sahihi na mtu atakayebainika kuleta madai ya kugushi atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kupelekwa mahakamani kwani hilo ni kosa la jinai.”alisema.
Disemba 28 mwaka jana Rais, Dk. Magufuli aliagiza vikokotoo vya zamani vya mafao ya wafanyakazi wa serikali pamoja na sekta binafsi katika mifuko ya hifadhi ya jamii viendelee kutumika kwa kila mfuko hadi mwaka 2023.
Katika maagizo yake Rais Magufuli alisema utaratibu wa zamani uendele kutumika ambapo wastaafu watapatiwa mafao ya mkupuo ya asilimia 50, kwa wastaafu wa serikali na asilimia 25 kwa wale wa sekta binafsi na sio kama ilivyopendekezwa katika kanuni mpya za ukokotoaji.
|
|
from Jamvi La Habari http://bit.ly/2LWEzxu
Tags
News
