Rais Trump awajia juu New York Times

Rais wa Marekani amesema kwa upande mmoja Marekani itaondoka Syria na kwa upande mwingine itaendelea kupambana na kundi la Daesh.

Rais Trump, kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter ameijibu makala iliyoandikwa na gazeti la New York Times iliyodai kwamba rais huyo anajichanganya katika suala la kuondoa majeshi Syria.

Rais wa Marekani Donald Trump, amesema vilaza wa New York Times pamoja na kujua nia yake wameandika makala ya kupotosha. Alichofafanua kuhusuiana na mchakato wa kuondoka Syria hakitofautia na alichokisema mwanzoni. kwamba wataendeleza vita dhidi ya Daesh na wataondoa majeshi nchini humo kwa kasi watayoona inafaa aliandika rais Trump.

Katika makala ya New York Times waliandika kwamba kuna mvurugano mkubwa kupita kiasi baina ya Trump na timu yake ya uongozi  kuhusiana na suala la kuondoka Syria. Gazeti hilo liliripoti kwamba uamuzi huo wa rais Trump umeikera sana wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon).

from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2GXfm78

Post a Comment

Previous Post Next Post