NA MWANDISHI WETU
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) kupitia madaktari wake bingwa wa magonjwa ya moyo kwa kushirikiana na Madaktari Afrika na Shirika la Cardio Start kutoka nchini Marekani wameanza kambi maalum ya siku 12 kwa ajili ya kutoa matibabu ya moyo
kwa watu wazima .
Kwa mujibu wa taarifa ya ofisa uhusiano wa JKCI,matibabu yatakayofanyika katika kambi hiyo ni upasuaji kufungua kifua na bila kufungua kifua.
Taarifa hiyo ilieleza kuwa Upasuaji wa bila kufungua kifua unafanyika kupitia tundu dogo linalotobolewa kwenye paja kwa wagonjwa kuzibuliwa mishipa ya moyo iliyoziba (Percutaneous Coronary Intervention – PCI) na kuwekewa vifaa vinavyosaidia kurekebisha mapigo ya moyo ambavyo ni (Permanent Pacemaker na High powered devices CRT-P, CRT –D) .
Ilieleza kuwa Wagonjwa watakaofanyiwa upasuaji ni wale wenye matatizo ya moyo ambayo ni valve, mishipa ya moyo iliyoziba, moyo kushindwa kufanya kazi vizuri, matibabu kwa watu wazima waliozaliwa na matatizo ya moyo na wale wenye matatizo ya moyo yaliyotokana na ugonjwa wa Kisukari
Kambi hiyo inayotarajiwa kuwahudumia wagonjwa 45 inaenda sambamba na utoaji wa elimu kwa madaktari na wauguzi pamoja na kubadilishana ujuzi wa kazi, kwa wageni na wataalamu wa nchini ilianza jana na inatarajiwa kuhitimishwa Januari 18 mwaka huu
Katika kambi hii tunatarajia kufanya upasuaji wa kufungua kifua kwa wagonjwa 20 na bila kufungua kifua kwa wagonjwa 25., hadi leo tarehe 8/1/2019 jumla ya wagonjwa nane wamefanyiwa upasuaji wa bila kufungua kifua na wagonjwa wanne wamefanyiwa upasuaji wa kufungua kifua.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kambi hiyo ni ya kwanza ya matibabu ya moyo tangu kuanza kwa mwaka wa 2019 ni mara ya kwanza kwa shirika Cardio Start kuja nchini kufanya kazi na JKCI.
from Jamvi La Habari http://bit.ly/2RBKnBS
