CCM watuma salamu za pole kufuatia kifo cha Ruge Mutahaba
Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetuma salamu za pole kwa familia ya Ruge Mutahaba ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Group (CMG).
Afya ya Ruge Mutahaba ilianza kutetereka katikati mwa 2018, na Juni mwaka huo alikwenda India kwa ajili ya matibabu na alirejea nchini Agosti 21, 2018. Baada ya muda kidogo hakuonekana, Oktoba 2018 alipelekwa Afrika Kusini kwa matibabu, amekaa huko hadi alipofariki.
Ruge Mutahaba amefariki siku ya jana nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu ya figo. Ruge alizaliwa mwaka 1970, Brooklyn nchini Marekani, atakumbukwa zaidi kwa mchango wake mkubwa katika sekta ya muziki nchini.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2BVPkfH
No comments