Breaking News

FIFA yamfungia maisha mwamuzi kutoka Tanzania


Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) imemfungia maisha mwamuzi wa zamani wa kimataifa ambaye pia ni Katibu wa Chama Cha Waamuzi Tanzania (FRAT) Oden Charles Mbaga kwa kujihusisha na masuala ya rushwa ya upangaji matokeo.

Aidha Mbaga anatakiwa kulipa faini ya kiasi cha fedha ya Uswis Faranga 200,000 (Zaidi ya shilingi milioni 468 a Kitanzania) ndani ya siku 30 tangu amepata taarifa hizo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na TFF, Uamuzi huo unafuatia uchunguzi uliofanyika kuanzia Julai 11, 2018 ambapo Mbaga amekutwa na hatia ya kuhusika kwenye upangaji wa matokeo ikiwa ni kinyume na kanuni za maadili za FIFA.

“Anafungiwa maisha kutojihusisha na shughuli zozote za mpira wa miguu katika ngazi ya Kitaifa na Kimataifa kwa mujibu wa Ibara ya 7j ya Kanuni za Maadili za FIFA za mwaka 2018 pamoja na Ibara ya 22 ya Kanuni ya Nidhamu ya FIFA,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Mwamuzi huyo anaweza kukata rufaa kwenye mahakama ya kimichezo ya FIFA (CAS) ndani ya siku 21 tokea maamuzi yalipofanyika na ndani ya siku 10 baada ya kumalizika siku 21.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2U9LTZZ

No comments