Breaking News

Kesi ya ubakaji ya Mstahiki Meya yaendelea kumsotesha rumande


Na. Thabit Madai Zanzibar

Kesi inayomkabili Mstahiki Meya wa Manispaa ya Magharibi ‘A’ mkoa wa Mjini Magharibi,
Hamza Khamis Juma kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 16 imepangwa
kusikilizwa Machi 13 mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Zanzibar.

Awali kesi hiyo ilianza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa wa Mjini Magharibi mbele ya
Hakimu wa Mahakama hiyo,Hamisuu Saaduni Makanjira.

Februari 14 mwaka huu mtuhumiwa huyo aliwasilisha maombi ya dhamana katika Mahakama hiyo ya Mkoa huo mbele ya Hakimu Hamisuu.

Mahakama hiyo ya mkoa ilishindwa kutoa dhamana kutokana na kutokuwa na uwezo wa kisheria ya kusikiliza maombi ya dhamana ya kesi hiyo.

Juma anakabiliwa na mashtaka mawili katika kesi hiyo ikiwemo kumtorosha na kumbaka mtoto huyo
wa kike mwenye umri wa miaka 16.

Katika kesi hiyo Meya huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 4 mwaka 2018 katika maeneo ya
Mwanyanya wilaya ya Magharibi 'A' mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.



from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2EC0h7U

No comments