Breaking News

MWAMUZI WA MECHI YA YANGA NA SIMBA HUYU HAPA


Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii

Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limemtangaza mwamuzi wa mchezo wa watani wa jadi ‘ Kariakoo Derby’ utakaopigwa kesho kwenye dimba la Uwanja wa Taifa

Mechi hiyo inayowakutanisha mahasimu wawili kati ya Simba na Yanga utachezeshwa na mwamuzi Hance Mabena kutoka Mkoani Tanga.

TFF, wamemtangaza Mwamuzi huyo Kijana kusimamia sheria 17 za mchezo wa soka baada ya kuonesha uwezo mkubwa kwenye michezo yake mengine

Mabena atasaidiwa na mwamuzi mkongwe Mohamed Mkono kutoka Mkoani Tanga na kijana Kassim Mpanga kutoka Mkoa wa Dar es Salaam.

Mwamuzi wa Akiba atakuwa ni Elly Sasii kutoka Mkoa wa Dar e Salaam.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utapigwa kesho kuanzia majira ya saa 10 alasiri kila upande ukijinasibu kuondoka na ushindi kwenye mechi hiyo.Yanga kinara wa TPL ana alama 58 huku watani wao Simba wakiwa nafasi ya tatu na alama 36 akiwa amecheza mechi 15 tofauti ya mechi zaidi ya sita na wapinzani wake


from MICHUZI BLOG

No comments