Naibu Waziri awaasa watumishi kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea
Watumishi wa Sekta ya Afya nchini wametakiwa kuacha tabia ya kufanya kazi kwa mazoea na wajikite katika kutoa huduma kulingana na sheria na taratibu za taaluma zao.
Hayo yamesemwa Leo na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati alipofanya ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za afya kwa Wananchi katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Ligula.
Katika ziara hiyo Dkt. Ndugulile amesema kuwa licha ya jitihada za kuboresha huduma za afya kwa Wananchi, ni wajibu wa kila mtoa huduma za afya nchini kuhakikisha anatimiza wajibu wake bila shurti na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
“Nyinyi mnafanya kazi kwa mazoea, kwa nini hamjajaza taarifa wala kusaini katika fomu ya wagonjwa, na hili linaendana na maelekezo ambayo Serikali tunawapa, kwamba kila mtu aandike tarehe na muda ambao amefanya kazi, nyinyi maabara hamfanyi” alisema Dkt. Ndugulile
Pia, Dkt. Ndugulile amesema kuwa Serikali imeboresha Vituo vya afya zaidi ya 300, ambavyo vitatoa huduma za dharura za upasuaji wakumtoa mtoto tumboni, na hospitali za wilaya 67, katika Mkoa wa Mtwara hospitali za wilaya 3 zinaenda kujengwa, ili kupunguza mzigo katika hospitali za mikoa,
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2GKbjdp
No comments