Breaking News

Rais Magufuli aguswa na kifo cha Ruge Mutahaba, aandika ujumbe mzito


Taarifa za kifo cha Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds Media Ruge Mutahaba, kimewagusa wengi mpaka Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Rais Magufuli ameonyesha kuguswa zaidi na msiba huo mkubwa na kuamua kutuma salamu zake za rambi rambi na pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia kifo cha Mkurugenzi huyo.

Rais Magufuli ametuma salamu hizo kupitia ujumbe aliouandika katika mtandao wake wa Twitter ikiwa ni muda mchache tangu kuanza kusambaa kwa taarifa za kifo cha Mkurugenzi huyo.

"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha kijana wangu Ruge Mutahaba. Daima nitamkumbuka kwa mchango wake mkubwa ktk tasnia ya habari, burudani, na juhudi za kujenga fikra za maendeleo kwa vijana," ameandika Rais Magufuli kwenye mtandao huo.

"Poleni wanafamilia,ndugu,jamaa na marafiki. Mungu amweke mahali pema, Amina,"ameongeza.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2GNahxm

No comments