SIMBA KUSHANGAZWA NA STAND UNITED
Licha ya kuifunga Lipuli FC jana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa bao 3-1. Uongozi wa Stand United umetuma salaam mapema za maangamizi kwa wekundu hao wa Kariakoo.
Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Stand, Athuman Bilal 'Bilo', amewataka Simba kujiandaa vema kisaikolojia wakienda kucheza na timu inayobutua mpira.
Bilo amewaambia Simba wao kama ni timu ya bilioni 1.3, wao hawajali hilo na watahakikisha wanawachukulia alama tatu kama walivyofanya kwa Yanga.
"Nawaambia kabisa Simba kuwa tutakapokutana nao Machi 3 wajiandae kushangazwa na wachezaji wetu wa ajabu, tutakutana Kambarage na tutawaonesha kuwa hatukubahatisha kwa Yanga", alisema.
Stand wanaenda kucheza na Simba Machi 3 kwenye uwanja wao wa nyumbani wa CCM Kambarage mjini Shinyanga.
from SALEH JEMBE
No comments