Breaking News

Wananchi watahadharishwa kuhusu Ugonjwa wa kimeta


Wananchi watahadharishwa kuwa makini wanaponunua nyama ya ng’ombe kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa kimeta na kuwataka kununua kitoweo hicho kwenye maeneo yaliyosajiliwa.

Vyombo vya habari vimeripoti juzi kutokea kwa vifo vya watu watano na ng’ombe 21 kwa ugonjwa huo wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro.

Kaimu Meneja Mkuu wa Kampuni ya Ranchi za Taifa (NARCO), Profesa Philemon Wambura amesema Ugonjwa huo ni hatari kwa kuwa ng’ombe anakufa ghafla akiwa amenona, hivyo watu wenye tamaa mbaya wanaweza kuuza nyama hiyo pasipo kujali athari zitakazojitokeza.

“Hatari inaweza kuwakabili zaidi wale wanaopenda kula nyama zisizokaguliwa ambazo haziuzwi kwenye maeneo rasmi yaliyosajiliwa, sasa wabadilike, waache kununua vichochoroni kuepuka shida zinazosababishwa na ugonjwa huo hatari,” alisema.

Alisema NARCO katika kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa iliyo bora wamekuwa wakihakikisha ng’ombe waliopo kwenye ranchi zao wanapata chanjo kwa wakati, pia kabla ya kuchinjwa wanakaguliwa ili kulinda afya za watumiaji wa nyama hizo.





from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2U62rBW

No comments