Yondani asifu kiwango alichoonyesha Kindoki
Beki mkongwe wa Yanga SC, Kelvin Yondani amesifu kiwango kilichoonyeshwa na kipa wa timu hiyo Klausi Kindoki huku akimtaka kutobweteka.
Yondani ameongea hayo ikiwa ni siku tangu kipa huyo aonyeshe kiwango kikubwa cha kuokoa michomo ya Namungo FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na Heritier Makambo.
Yondani amesema kuwa Kindoki ni kipa mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kudaka, lakini presha ya mashabiki ndiyo imemfanya apoteze hali ya kujiamini akiwa golini.
“Kindoki siyo kipa mbaya ni mzuri na nilianza kumuona tangu alipojiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu, kosa kubwa alilolifanya aonekane siyo mzuri ni kupoteza hali ya kujiamini baada ya kufungwa michezo ya mwanzoni, lakini sasa ameshawaonyesha watu kuwa yeye ni hatari sana.
Hata hivyo ameongeza kuwa anachotakiwa ni kuwajua mashabiki na kuongeza hali ya kujiamini ili akontroo presha kama alivyofanya katika mchezo uliopita wa Kombe la Shirikisho walipocheza na Namungo, kiukweli alidaka vizuri.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2BV55nf
No comments