Breaking News

Serikali yapongezwa kushughulikia tatizo la umeme na simu



Na.Ahmad Mmow, Nachingwea.

Serikali imepongezwa na kushukuriwa kwa kushughulikia tatizo la umeme na mawasiliano ya simu katika kata ya Matekwe na tarafa ya  Kilimarondo.

Pongezi na shukrani hizo zimetolewa leo na aliyekuwa kamishna wa mkoa wa Lindi wa chama cha Alliance for Democratic Change(ÀDC),Haji Nanjase alipozungumza na Muungwana blog kijijini Matekwe.

Nanjase ambae aliweka wazi kwamba kwasasa sio kiongozi wa chama chochote cha siasa,bali alizungumza kwaniaba ya wapenda maendeleo,alisema alikuwa nakila sababu ya kuipongeza serikali kwa kushugulikia matatizo hayo ambayo hakuna aliyekuwa anatarajia kama yatashugulikiwa.

Alisema tatizo la mawasiliano limeshughulikiwa katika kijiji hicho,kata ya Matekwe,Kiegei na Kilimarondo. Kwani tayari wananchi wanatumia simu za mikononi kwa mawasiliano kupitia kampuni za Vodacom na TTCL.

Aidha kuhusu tatizo la umeme,Nanjase ambaye sasa ni mwenyekiti wa chama cha msingi cha ushirika cha New Matekwe(New Matekwe AMCOS),alisema serikali imeanza kushughulikia. Ambapo mafundi wanaendelea na kazi ya ujenzi wa miundombinu ya umeme utakao tumia nguvu za jua katika kijiji cha Matekwe.

"Mbali na hayo lakini tayari serikali imekarabati kituo cha afya cha Kilimarondo na nyumba za watumishi.Hata watumishi wa serikali wanaletwa.Sasa nilazima niipongeze serikali kama mpenda maendeleo,"alisisitiza Nanjase.

Nanjase pia aliishukuru serikali kwa kuboresha huduma za matibabu kwenye zahanati. Hali ambayo inasababisha wananchi kuwa na uhakika wa tiba.

Alisema kila mpenda maendeleo hawezi kusita kuipongeza na kuishukuru serikali kwani huduma hizo zitachochea maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wanaoishi kwenye kata hizo.

Kata za Matekwe, Kilimarondo na Kiegei ni miongoni mwa kata zenye umbali mrefu kutoka mjini Nachingwea palipo makao makuu ya wilaya ya Nachingwea. Hata hivyo hazikuwa na mawasiliano ya simu.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2VUQO1j

No comments