Usalama yabaki daraja la pili, Ihefu SC yasonga daraja la kwanza
Na. John Walter, Babati
Usalama Sc ya mkoa wa Manyara iimeendelea kubaki katika ligi daraja la pili msimu wa 2019/2020 baada ya kufanya vibaya katika michuano hiyo iliyofikia tamati jumapili March 10.2019.
Katika mchezo wao wa mwisho Usalama Sc ilikuwa nyumbani katika uwanja wa shule ya Sekondari Singe mjini Babati ambapo walimkaribisha Ihefu Sc kutoka Mbeya.
Usalama Sc ikiwa nyumbani imekubali Ihefu Sc wasonge mbele ligi daraja la kwnza kibabe kutoka nyuma kwa mabao 2-0 hadi kufikisha 3-2 kipindi cha pili dakika za lala salama.
Baada ya mchezo kumalizika kocha wa Usalama Sc Henry Mkanwa na meneja wake waligoma kuzungumza na waandishi wa habari kwa maelezo kwamba kuna msemaji ambapo hata hivyo hakuwa uwanjani hapo.
Kocha huyo amekuwa akiumiza kichwa namna ya kupata matokeo bila mafanikio jambo linaloonekana kumkosesha raha kila inapokutana na mpinzani kwa kuwa wameokuwa wakipata matokeo mabaya wakati wote.
Kocha wa timu ya Ihefu Sc Salhina Mjengwa,anasema licha ya uchovu waliokuwa nao wanamshukuru Mungu kwa kupata matokeo hayo dhidi ya Usalama na kinachofuata kwa sasa ni maandalizi ya ligi daraja la kwanza msimu unaokuja.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2u3pQsz
No comments