Waziri Jafo awapa tahadhari, 'Msije kuingizwa mkenge'
Wazri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ametembelea ujenzi wa upanuzi wa kituo cha afya Mlandizi na hospitali ya wilaya inayojengwa Kibaha Vijijini, na kutaka hospital hizo zikamilike kwa muda huo na kwa kiwango chenye ubora kulingana na thamani iliyotolewa.
Alisema serikali imetoa kiasi cha sh. milioni 400-500 kwa vituo vya afya 97 nchini ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Pia aliyaasa mashirika yasiyo ya kiserikali ikiwemo TACAIDS kukabidhi fedha za miradi wanayotaka kuyajenga ikiwemo maabara katika kituo cha afya Mlandizi kwa halmashauri ya Kibaha Vijijini badala ya kusimamia wenyewe ili kuondoa mkanganyiko.
“Kwanini mkandarasi wamlete wao, nyie wenyewe mmeweza kujenga kwa umakini na kutumia fedha vizuri kuboresha kituo hiki cha afya, kwanini wao wasitoe hizo milioni 600 kwenu mkasimamia miradi hiyo “
“Msije kuingizwa mkenge simamie na wanapaswa kupitisha fedha hizo kwenu," alisisitiza Waziri Jafo.
Katika hatua nyingine Waziri Jafo ameziagiza halmashauri zote nchini zilizopatiwa fedha za kujenga hospitali ya wilaya mpya, kuhakikisha wanasimamia majengo hayo yanakamilika ifikapo Juni 30 mwaka huu.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2u20bQM
No comments