Breaking News

AKILIMALI AJA JUU, ATAKA SIMBA NA KMC WAPEWE ALAMA MOJA MOJA, ADAI MATOKEO YALIPANGWA


Mjumbe wa Baraza la Wazee katika klabu ya Yanga, Ibrahim Akilimali amelitaka Shirikisho la Soka Tanzania kugawa alama moja kwa Simba na KMC baada ya mchezo wa jana.

Akilimali amesema kama TFF wamemfungia Kambuzi na wasaidizi wake waliochezesha mchezo wa jana basi na maamuzi yabadilishwe ili kuweka usawa.

Ameeleza kuwa mechi hiyo ilipaswa kwenda sare ya bao 1-1 lakini kufeli kwa waamuzi kulisababisha KMC wanyimwe penati na badala yake wakapewa Simba baadaye.

Hata hivyo, Akilimali amesema kuwa anajua bingwa wa msimu huu ameshapangwa hivyo wala hapepesi kuumiza kichwa hivi sasa.

"Unajua hawa TFF wanapaswa kuwapa Simba alama moja pamoja na KMC kwa sababu mechi hiyo ilipaswa kumalizika kwa sare ya 1-1.

"Kilichofanyika ni kuibeba tu Simba na TFF wanapaswa kubailisha maamuzi baada ya kuwafungia Kambuzi na wenzake kwa makosa ya uwanjani.

"Najua bingwa ameshapangwa kwa hiyo sioni tatizo na wala siumizi kichwa juu ya nani aatachukua kikombe."

from SALEH JEMBE

No comments