Breaking News

EU yaikosoa Urusi kwa kuwapa Waukraine uraia


Umoja wa Ulaya leo umeikosoa vikali hatua ya Urusi kuharakisha maombi ya uraia kutoka kwa watu wanaoishi katika maeneo ya migogoro mashariki mwa Ukraine, na kuitaja kuwa ni shambulizi dhidi ya uhuru wa Ukraine ambalo litahujumu makubaliano ya amani ambayo tayari ni tete.

Rais wa Urusi Valdmir Putin alisaini amri jana ya kuyashughulikia katika kipindi cha miezi mitatu maombi ya uraia kutoka kwa baadhi ya Waukraine wanaoishi katika maeneo yanayodhibitiwa na wapiganaji wanaotaka kujitenga ambao wanaungwa mkono na Urusi.

 Watakaopewa uraia wa Urusi watahitajika kuapa kuwa watiifu kwa Urusi. Katika taarifa ya pamoja, Ufaransa na Ujerumani - ambazo ndizo nchi za Ulaya zilizosimamia utiaji saini wa muafaka wa amani wa Minsk mwaka wa 2015 - zimesema kuwa amri hiyo inakwenda kinyume na madhumuni ya makubaliano hayo ya Minsk.

from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2UF7vwP

No comments