KIONGOZI YANGA: TFF WALIUMIZWA NA MATOKEO KAGERA WAKAPANGA MATOKEO MECHI NA KMC
Wakati kikosi cha Simba kikishuka dimbani Uwanja wa Karume leo kumenyana na Biashara kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara, Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali, amesema kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) liliumizwa na matokeo ya timu hiyo mkoani Kagera.
Akilimali amesema kuwa baada ya Simba kufungwa na Kagera mabao 2-1 na kuamua kupanga matokeo ya mchezo uliofuata na KMC FC uliopigwa Uwanja wa CCM Kirumba.
Mzee huyo ameeleza TFF iliyo chini ya Rais Wallace Karia haikuwa na wakati mzuri baada ya kupoteza mbele ya Kagera na ili mipango isiharibike waliamua kupanga mechi dhidi ya KMC kuipa urahisi wa kushinda.
Katika mechi dhidi ya KMC Simba walifanikiwa kushinda kwa mabao 2-1 huku penati ya ushindi kwa Simba ikileta gumzo kubwa kwa namna ilivyopatikana.
Akilimali alieleza kuwa penati hiyo ilikuwa ya mipango na badala yake akasema mchezo huo haukuwa na maana yeyote kwani tayari ulikuwa una matokeo kabla ya kuchezwa.
from SALEH JEMBE
No comments