Breaking News

LIONEL MESSI AJIJENGEA UFALME WAKE, AMPOTEZA BENZEMA NA RONALDO KWA KUCHEKA NA NYAVU


MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi amewejiwekea ufalme wake kwa kucheka na nyavu ndani ya La Liga baada ya kufikisha jumla ya mabao 33 kwa sasa kwenye ligi hiyo huku akimuacha mbali mpinzani wake wa Real Madrid Karim Banzema mwenye mabao 21.

Messi amecheza dakika 2485 na anawastani wa kupachika bao moja kila baada ya dakika 75 akiwa ndani ya uwanja huku akitoa jumla ya pasi 13 zilizoleta mabao kwa timu yake ambayo imefunga jumla ya mabao 83.

Upande wa Benzema yeye amecheza dakika 2795 akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 133 akiwa uwanjani na timu yake imefunga jumla ya mabao 59.

Kwa upande wa Cristiano Ronaldo ambaye yupo Ligi Kuu ya Italia akikipiga Juventus ametupia jumla ya mabao 19 na ametoa pasi 8 za mabao huku akicheza jumla ya dakika 2329 ana wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 123.



from SALEH JEMBE

No comments