Rais wa Urusi asifu mpango wa China kuimarisha miundombinu
Rais wa Urusi Vladimir Putin ameusifu mpango wa China wa kuimarisha miundombinu akitilia mkazo mahusiano mazuri yaliyopo kati ya mataifa hayo yenye nguvu.
Putin amewambia zaidi ya viongozi 40 wanaohudhuria mkutano mjini Beijing kuwa mpango huo wa China unalenga kuimarisha ushirikiano wa mataifa ya Ulaya na bara Asia.
Matamshi hayo yanaashiria kuondoa uwezekano wa kuzuka mivutano kati ya Urusi na China na mshikamano wa pamoja wa mataifa hayo dhidi ya ushawishi wa Marekani duniani.
Mpango huo wa kufadhili barabara na miundombinu mingine unaojulikana kama Belt and Road tayari umetanua ushawishi wa kiuchumi wa China kwenye kanda ya Asia ya Kati eneo ambalo Urusi imekuwa na ushawishi wake kwa muda mrefu.
from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2VvCrUw
No comments