Breaking News

RUNGU LAWAANGUKIA WAAMUZI WALIOTOA PENALTI MBILI KWA SIMBAM WAFUTWA KAZI


BAADA ya Jana kushindwa kuumudu mchezo kati ya KMC na Simba, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limewapiga pini waamuzi hao kwa kuchezesha mchezo huo chini ya kiwango.

Katika mchezo huo ambao Simba ilishinda kwa mabao 2-1 huku wakipewa penalti mbili ambayo moja ilikoswa na Meddie Kagere na ya pili ikafungwa na John Bocco uwanja wa CCM Kirumba.

(TFF), imewaondoa kwenye orodha ya waamuzi wa msimu huu, Abdallah Kambuzi, Godfrey Msakila na Consolata Lazaro ambao walichezesha mchezo huo wa KMC na Simba jana Aprili 25, 2019.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na shirikisho hilo, waamuzi hao wameondolewa kuchezesha mechi zilizosalia za Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu baada ya kuonesha kiwango kisichoridhisha kwenye mchezo huo.

Katika mchezo huo Kambuzi alikuwa mwamuzi wa katikati akisaidiwa na mwamuzi msaidizi namba moja Godfrey Msakila na mwamuzi msaidizi namba mbili Consolata Lazaro.

Katika taarifa hiyo, TFF imewaonya waamuzi wote wa ligi kuu, ligi daraja la kwanza na daraja la pili kuwa makini “Yeyote atakayebainika kuchezesha chini ya kiwango kwa namna yoyote atakuliwa hatua stahiki”, imeeleza taarifa hiyo.


from SALEH JEMBE

No comments