Breaking News

Watawa wahukumiwa kunyongwa kwa mauaji ya Askofu


Watawa wawili wa kiume wa Kanisa la Khufti (Coptic) wamehukumiwa kifo nchini Misri kwa mauaji ya Askofu Epiphanius (64)mwaka 2018.

Askofu Epiphanius alipatikana akiwa ameuawa na kuvuja damu nyingi ndani ya makazi ya kanisa Kaskazini Magharibi mwa jiji la Cairo mwezi Julai 2018.

Mamlaka za Misri zilihusisha tukio hilo na ugomvi ambao haukuwekwa wazi baina ya watawa hao na askofu Epiphanius.

Mmoja wa watawa hao, Wael Saad, ameripotiwa kukiri mbele ya waendesha mashtaka kuwa alitumia nondo kumshambulia Askofu huyo mpaka kufikwa na umauti na mtawa Remon Rasmi, alishtakiwa kwa kosa la kumpatia Saad usaidizi

from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2VqgXsj

No comments