Waziri aagiza stendi ya Njombe kuanza kutumika tarehe 10
Na Amiri kilagalila-Njombe
Naibu waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh.Joseph Sinkanda Kandege ameiagiza halmashauri ya mji wa Njombe kuhakikisha kituo kipya cha mabasi kinacho jengwa mjini Njombe kuanza kutumika mapema tarehe kumi mei bila kupitisha agizo la Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.
Waziri ametoa agizo hilo hii leo wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa stendi hiyo huku akiridhishwa kutokana na kazi ambazo zimefanyika na kufikia hatua nzuri ya ujenzi na kuwataka mara moja kuanza kuwatangazia wananchi mara moja bila kubadilisha maagizo ya Rais.
“kwa kazi ambazo zimefanyika mimi niwapongeze lakini tarehe kumi mwezi mei stendi naomba ianze kutumika bila ya kuwa na maneno mengine yoyote ya kujitetea,na ni vizuri mkaanza kuwatangazia wenye mabasi na wenye daladala kama ambavyo mheshimiwa Rais aliwaomba wananchi wavumilie kipindi cha siku 30 hakuna namna ambavyo tunaweza kuyabadilisha maneno yale na kwa kazi ilipofikia hakuna sababu ya kuto kuanza kuitumia stendi hii”alisema Kandege
Kwa upande wake mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe Iluminata Mwenda amesema kuwa stendi hiyo itaanza kutumika mapema baada ya kukamilika.
“stendi hii tutaikamilisha ndani ya muda tuliopewa na Rais na itaanza kutumika mala moja na sasa tumeshaanza kukutana na wadau mbali mbali kwa ajili ya kuweka utaratibu”
from MUUNGWANA BLOG http://bit.ly/2L3tAoX
No comments