Breaking News

Lipumba: Kifo cha Khalifa ni pengo kubwa CUF


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema kifo cha katibu  mkuu wa chama hicho, Khalifa Suleiman Khalifa kimeacha pengo kubwa katika chama hicho.

Khalifa ambaye amewahi kuwa mbunge wa Gando kuanzia mwaka 1995  hadi 2015 amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Jumanne Machi 31, 2020  katika hospitali ya Aga Khan alikokuwa akipatiwa matibabu.

Profesa Lipumba ameeleza hayo leo Jumanne Machi 31, 2020 wakati akizungumza na Mwananchi.



from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3bCNq2R

No comments