Meneja wa Diamond apona Corona
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Sallam SK ameweka wazi kuwa sasa ni mzima baada ya siku 14 alizokuwa ametengwa kwa ajili ya matibabu kumalizika.
Sallam ambaye ni meneja wa Diamond Platnumz amesema amefanyiwa vipimo mara kadhaa ya vyote vimeonesha kuwa hana tena maambukizi ya virusi vya corona.
Kupitia instagram ameandika hivi;
Nimshukuru Allah 🙏🏽 na pia niwashukuru wote mlionitumia msg, comments, DM na dua zenu. Bila kuwasahau Temeke Isolation Centre kwa kuwa bega na bega pamoja na mie bila kunichoka pale nilipokuwa nimezidiwa, na shukurani zangu zingine ziende kwa Madaktari bingwa kujua maendeleo yangu mara kwa mara na pia Serikali yangu na viongozi wake husika Wizara na Mkoa walikuwa hawana ubaguzi kutujulia hali na kutupa moyo na kutupa mahitaji tutakayo. Naomba niwape taarifa ndugu yenu, kijana wenu nimechukuliwa vipimo mara mbili na nimekutwa NEGATIVE na kwa sasa nipo huru. Ila naomba tuendelee kujikinga na kufata ushauri wa viongozi wetu na kuacha maelekezo ya utashi yasiyokuwa na uhakika. ALLAH IS GREAT 🙏🏽🙏🏽🙏🏽
Machi 19 mwaka huu alibainika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo vinavyosababisha homa ya mapafu, baada ya kutembelea nchi ambazo tayari zilikuwa na maambukizi.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2xGA9Yk
No comments