Breaking News

Asilimia 60 ya abiria waliokwama katika meli Uruguay wakutwa na maambukizi ya corona

Abiria waliopo kwenye Meli ya Greg Mortimer iliyokua inatoka Australia kwenye Antarctica , Wamejikuta katika wakati mgumu Baada ya Meli hiyo kuzuiwa katika Bandari ya Uruguay huku asilimia 60 kati yao wakithibitika kua na Maambukizi ya COVID-19. .

Kati ya Abiria 217 waliopo kwenye Meli hiyo, Abiria 128 wamepimwa na kukutwa na Virusi vya Corona, huku Abiria 6 wakiwa katika hali mbaya Zaidi. .

Hata hivyo Tayari utaratibu umefanyika ili kuwatoa Abiria ambayo hawajaambukizwa , huku Abiria wote ambao Tayari wameathirika watahitajika kupewa huduma ndani ya Meli hiyo mpaka watakapopona. Meli hiyo ilianza Safari yake toka March 15 mwaka huu. .

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2y1m0oJ

No comments