Breaking News

Conte atoa ombi jipya la hati fungani za Umoja wa Ulaya za kufufua uchumi


Waziri mkuu wa Italia Giuseppe Conte leo ametoa ombi lingine kwa Umoja wa Ulaya kubuni mipango maalumu ya kuanzisha mpango wa kihistoria hati za dhamana, wakati ambapo mataifa yakitafuta jawabu la pamoja kuhusu kudorora kwa uchumi na ukosefu wa ajira.

 Conte alitoa wito wa ''hati za dhamana za kuchochea uchumi wa umoja wa Ulaya'' katika tahariri ya gazeti la Repubblica akijibu barua ya rais wa halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen aliewaahidi raia wa Italia msaada zaidi kutoka Umoja huo katika toleo la jana la gazeti hilo.

 Ujerumani na Uholanzi zinapinga kubuniwa kwa mpango huo zikisema utafanya mataifa kuwa na jukumu katika madeni ya mataifa mengine. Italia na Uhispania zinazoungwa mkono na mataifa mengine ikiwa ni pamoja na Ufaransa, zinaongoza katika mchakato huo.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2xQ9wk4

No comments