Breaking News

Marekani yatoa mpango wa mpito kwa Venezuela

Serikali ya Marekani imesema kuwa iko tayari kuiondolea vikwazo Venezuela kuunga mkono pendekezo jipya la kuunda serikali ya mpito inayowahitaji rais Nicolas Maduro na kiongozi wa upinzani Juan Guaido kukaa kando na kutoa nafasi kwa baraza la uongozi la wanachama watano.

''Mpango huo wa mpito wa kidemokrasia wa Venezuela'' wa ukurasa mmoja, ulitolewa jana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo.

Hatua hiyo inaonekena kutilia mkazo pendekezo lililotolewa mwishoni mwa juma na Guaido linaloonyesha jinsi hofu kuhusu virusi vya corona inavyotishia kutatiza mifumo ya kiafya na kiuchumi ambayo tayari imesambaratika katika taifa hilo la Amerika Kusini inavyofufua juhudi za Marekani za kuliondoa jeshi kutoka upande wa Maduro.

Pompeo amesema kuwa mpango huo unaweza kutoa mwelekeo wa kumaliza mateso na kufungua njia za maisha bora katika siku zijazo nchini humo.



from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3dN2s8d

No comments