Mkuu wa Mkoa wa Rukwa awataka waganga, machifu kupambana na corona
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joachim Wangabo amewaagiza machifu pamoja na waganga wa tiba asili ndani ya mkoa huo kupambano dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona, kwa kuwa na ndoo za maji yanayotitirika na sabuni katika maeneo yao ya kazi.
Ametoa maagizo hayo katika kikao kifupi kilicholenga kutoa elimu ya ugonjwa wa virusi vya Corona kwa machifu pamoja na viongozi wa waganga wa tiba asili wakiwemo wa Chama cha Waganga/ Wakunga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala Mkoani Rukwa (CHAWATIRU).
Amesema kuwa haitakuwa na maana kama wamepata elimu halafu hawaitumii hali ambayo hakutakuwa na wa kumlaumu endapo ugonjwa huo utasambaa na kuangamiza watu, huku akisisitiza kuwaelimisha wateja wao na kushindwa kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ni sawa na kulisaliti taifa.
“Kwa upande wa maji mimi kwangu ni agizo, machifu wote muwe na ndoo ya maji tiririka na sabuni, muoneshe mfano, waganga wa tiba za asili na nyinyi wote kwa umoja wenu mkawe na ndoo za maji tiririka na sabuni na elimu mmeipata vizuri. Haitakuwa na maana kama mmepata elimu halafu kule mnakwenda hamuitumii halafu ugonjwa unakuja unatuangamiza, utamlaumu nani na elimu tumekupa, itabidi ujute kwamba wewe ni msaliti na umelisaliti taifa, umemsaliti na Mungu pia,” amesema RC Wangabo.
Mhe. Wangabo aliwataka machifu hao kukemea mila zinazowezesha kusambaa kwa ugonjwa wa Corona kwa haraka, ikiwemo watu zaidi ya mmoja kutumia chombo kimoja kunywa pombe za asili, familia kutumia chombo kimoja kutumbukiza mikono kwaajili ya kunawa, pamoja kutumia chombo kimoja cha kuchotea na kunywea maji katika mtungi.
Halikadhalika aliwataka waganga wa tiba asili kuwa na utatratibu wa kulipwa kwa kutumia huduma za mitandao ya simu ama benki ili kuepuka kushika fedha za wagonjwa ambao hawajulikani huku akisisitiza kutotowa dawa zinazopelekea mtu kupiga chafya kwa wingi jambo ambalo sio zuri hasa katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Corona.
Kwa upande wake, kaimu mganga Mkuu wa mkoa wa Rukwa Dkt. Emanuel Mtika aliwatahadharisha kuwa kuwatibu wagonjwa wa Corona ni gharama kubwa sana kiasi ambacho endapo ugonjwa huo utasambaa watu wengi wanaweza kupotea kwa kushindwa kufuata maelekezo ya wataalamu.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/34hWqYU

No comments