Nyota ya Samatta yazidi kung'aa, klabu ya Galatasaray ya Uturuki yamtaka
Nyota wa kimataifa wa Tanzania anayekipiga Aston Villa ya Ligi Kuu England, Mbwana Samatta, huenda akatua Galatasaray ya Uturuki iliyoonyesha nia ya kuhitaji huduma ya straika huyo wa zamani wa Simba.
Hata hivyo, Galatasaray inafuatilia mwenendo wa Aston Villa na kwamba iwapo klabu hiyo itashuka daraja, watatumia mwanya huo kumtwaa Samatta. Samatta aliyejiunga na Aston Villa Januari mwaka huu akitokea Genk ya Ubelgiji, amefunga mabao mawili na timu yake hiyo mpya katika mechi za Ligi Kuu England.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa jana na
Fotospor, Galatasaray pia walikuwa wakimwania Samatta kipindi cha dirisha dogo la Januari, lakini walipigwa kikumbo na Aston Villa, hivyo kwa sasa wanajipanga kumnasa usajili wa kiangazi.
Miamba hiyo ya soka Uturuki, inaamini Villa watakuwa tayari kuwauza wachezaji wao iwapo wakali hao wa England watashuka daraja.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2Jx4s6K

No comments