Breaking News

Rotimi afunguka kuhusu penzi lake na Vanessa Mdee “Hatuachani”

Mwimbaji Staa wa Bongofleva Vanessa Mdee amevunja ukimya kwa kuongelea ukimya wake na maamuzi yake ya kupumzika.

“Kwa miaka 13 nimefanya kazi bila mapumziko, hatimae nimepata muda kwa ajili yangu, kufanya ninavyovipenda na kuvitaka, nataka kuchukua muda kufurahia maisha, tuko hapa kwa ajili ya kuishi na kufurahia maisha” – Vanessa Mdee

Wakati Vanessa akiongea kwenye hii video na kuonesha kufurahia penzi lake jipya na Mwigizaji Staa Rotimi, Mpenzi wake huyo alijitokeza na kuongea kwa kiswahili kurudia kwa msisitio neno ‘hatuachani’

Vanessa amewashukuru Mashabiki zake pia kwa kusupport podcast yake kwenye season ya kwanza na kuahidi kuileta season ya pili na kujibu maswali mengi ya Mashabiki zake.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2UX0U2C

No comments