Taliban yawatuhumu Marekani na washirika wake kwa kukiuka mkataba wa Doha
Kundi la wanamgambo wa Taliban hii leo limeituhumu Marekani na washirika wake kwa kuyakiuka makubaliano ya Doha yaliyosainiwa mwezi mmoja uliopita katika mji huo mkuu wa Qatar.
Hata hivyo jeshi la Marekani nchini Afghanistan linakana madai hayo ya Taliban. Kwenye taarifa yake, Taliban inaorodhesha ukiukwaji huo kuwa ni pamoja na kutoachiwa huru wafungwa 5,000 wa kundi hilo, mashambulizi kwenye makambi yake na kuendelea kwa uvamizi na mashambulizi ya kutokea angani dhidi yao yanayofanywa na vikosi bya Marekani na Afghanistan.
Taliban inaonya kwamba hatua kama hizo zinaweza zikavuruga makubaliano na kuchochea machafuko yanayofanywa na wanamgambo hao.
Sehemu ya taarifa yao imesema wanamgambo hao wanawaomba Wamarekani kuheshimu maudhui ya makubaliano hayo lakini pia wawaarifu washirika wao pia kuutekeleza kikamilifu mkataba huo.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2xMZksp
Taliban yawatuhumu Marekani na washirika wake kwa kukiuka mkataba wa Doha
Reviewed by Tanzania Yetu
on
April 05, 2020
Rating: 5

No comments