Breaking News

VIDEO: Wananchi wafuate maelekezo na ukiona Polisi wanaingia mtaani ni kwa ajili ya ulinzi - IGP Sirro


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro, amesema kuwa Jeshi la Polisi kamwe halitamvumilia mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo kujihusisha na uuzaji na usambazaji wa dawa za kulevya pamoja na uhalifu mwingine.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati akifungua kituo cha utalii Nungwi mkoa wa Kaskazini Unguja kisiwani Zanzibar, huku akiwataka watendaji wa Jeshi la Polisi nchini kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa weledi na kwa kufuata misingi ya kisheria na kufuata maelekezo ya Jeshi hilo.


IGP Sirro ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kufuata maelekezo mbalimbali yanayoendelea kutolewa na viongozi wa kiserikali pamoja na wataalamu wa masuala ya afya.

TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI.....USISAHAU KUSUBSCRIBE



from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2w4hrtr

No comments