Watoto 10 waliozaliwa katika hospitali moja Romani wapatikana na virusi vya corona
Uchunguzi unaendelea kuhusu kitengo cha uzazi katika hospitali moja nchini Romania baada ya watoto kumi waliozaliwa kupatikana wana virusi vya corona.
Inakisiwa kwamba waliambukizwa virusi hivyo na wahudumu wa afya katika hospitali hiyo.
Kulingana na waziri wa afya wa Romania Nelu Tataru, wazazi wa watoto hao wamepimwa na kupatikana hawana virusi hivyo vya corona.
Inaripotiwa kwamba watoto hao hawaonyeshi dalili zozote za ugonjwa wa covid-19.
Kisa hiki kinatia wasiwasi kuhusiana na jinsi mfumo wa taifa la Romania unavyolishughulikia janga la virusi vya corona.
Katika wiki za hivi majuzi wahudumu wa afya wamelalamikia ukosefu wa vifaa vya kujikinga wanapokuwa kazini.
Kuna zaidi ya visa elfu nne vya maambukizi Romania kwa sasa na watu 180 wameaga dunia.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2Xh2CPd

No comments