Breaking News

DC Komba awaonya wafanyabiashara


Na Ahmad Mmow, Lindi.


Mkuu wa wilaya ya Nachingwea, mkoa wa Lindi, Hashimu Komba amewaonya wafanyabishara wilayani humo wasiuze sukari kwa zaidi ya shilingi 2,800 kwa kila kilo moja.

 Komba alitoa onyo hilo jana alipozungumza kwa simu na Muungwana Blog toka Nachingwea kueleza jinsi  serikali wilayani humo inavyodhibiti mfumuko wa bei ya sukari.

Alisema wafanyabiashara wilayani humo hawana sababu ya kuuza sukari kwa zaidi ya shilingi 2,800 kwani baada ya kukokotoa gharama ya ununuzi na usafirishaji amebaini kwamba hawanasababu ya kuuza kwa zaidi ya shilingi 2,800.

 Komba amesema ni jambo lisilokubalika wala kuvumilika kuona wafanyabiashara anauza bidhaa hiyo kwazaidi ya shilingi 2,800 wakati wakiuza kwa bei hiyo ya shilingi 2,800 wanapata faida.

 '' Niwaombe sana sana, katika kipindi hiki cha mfungo kuna wafanyabiashara wanapandisha bei za vyakula ghafla. Marufuku kuuza sukari kwa shilingi 3,000,'' alisisitiza Komba.

Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya Kilwa, Christopher Ngubiagai akiongoza operesheni maalum wilayani Kilwa aliwatia mbaroni wafanyabiashara 14 kwakuuza sukari kwa bei za kulangua  ambazo zinawaumiza walajiwa.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2SPSIBg

No comments