Breaking News

RC Ruvuma awageukia madiwani na watendaji walio sababisha manispaa ya songea kupata hati isiyo ridhisha


Na Muhadh Mohammed.


MKUU wa Mkoa wa Ruvuma Christin geta Mndeme ameuagiza uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Songea kuwachukulia hatua za kinidhamu watumishi au madiwani waliosababisha hati ya mashaka katika manispaa hiyo .

Hatua hiyo imekuja kufuatia mkaguzi wa hesabu za Serikali(CAG) kubaini baadhi ya hoja kushindwa kujibiwa ikiwemo ya upotevu wa  fedha wa sh.Milioni 98  katika mwaka wa fedha 2018 na 2019.

 Mndeme ametoa maagizo hayo jana kwenye kikao cha baraza la Madiwani la Manispaa hiyo ambalo lilikuwa rasmi kwaajili ya kupokea maelekezo ya mkuu huyo kufuatia upataji wa hati hiyo na namna ya kujipanga ili isijirudie tena.

  Kufuatia hali hiyo mkuu huyo ameutaka uongozi wa Halmashauri kuwachukulia hatua za kinidhamu wale wote waliosababisha upataji wa hati hiyo bila kujali vyeo vyao au nyazifa zao ili kukomesha vitendo hivyo visijirudie kwa mwaka mwingine wa fedha.

Mkuu huyo amesema kuwa ofisi yake ya mkoa  imesikitishwa na upatikanaji wa hati hiyo ya mashaka kwa kuwa Manispaa ya Songea ndiyo kioo cha mkoa mzima ndani ya Ruvuma na ina vyanzo vingi vya mapato ambayo yakisimamiwa hati hiyo isingeweza kupatikana.

“Haiwezekani Rais wetu Dkt ,John Pombe Magufuli anahangaika namna ya kuwasaidia wananchi hasa wanyonge sisi huku tunafanya madudu ya kuiumiza Serikali nasema sitakubali lazima hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi ya waliosababisha hati hiyo”amesema mkuu huyo Christina Mndeme.

  Kwa upande wake mkaguzi wa Nje wa hesabu za Serikali mkoani humo Deogratius Peter amesema Halmashauri hiyo imepata hati hiyo kutokana na sababu  moja tuu ya fedha ya sh.Milioni 130  za mapato ziliibiwa zikarejeshwa  baadhi ya fedha na kubakia kiasi cha sh.Milioni 98 na zikaingizwa kama sehemu ya mapato wakati hazipo jambo ambalo limepelekea dowa  kwenye ripoti za hesabu za serikali.

 Hata hivyo mkaguzi huyo amependekeza waliyohujumu fedha hizo wachukuliwe hatua za kisheria ili kudhibiti vitendo hivyo visiendelee kwa watumishi wengine ,huku akiwataka madiwani kupitia vikao vyao waweze kuifuta fedha hiyo kwenye vitabu vyao kwa kuwa fedha hizo hazitarudi kwenye Halmashauri bali zitaenda chanzo kikuu.

  Naye Meya wa Manispaa hiyo Abdul Mshaweji akipokea maagizo hayo amesema kuwa atayafanyia kazi ili jambo hilo lisiweze kujirudia katika kipindi kijacho.

from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2LhxjN1

No comments