Breaking News

RC KNENGE AWATAKA WAKAZI WA NGOMA MAPINDUZI KUTOVAMIA MAENEO YALIOACHWA WAZI

Na Agness Francis, Michuzi Tv

MKUU wa Mkoa waDar es Saalam Aboubakar Kunenge ametembelea mradi wa KC land development plan inayotoa mikopo ya viwanja kwa muda mrefu bila riba,Uliopo kijiji cha Ngoma Mapinduzi  halmashauri ya wilaya ya kigamboni  Jijini Dar es Salaam, Sanjari na kuzindua visima vya maji safi na salama kwa wananchi hao waliikuwa na kiu ya huduma hiyo kwa muda mrefu.

Aidha baada ya khafla ya uzinduzi huo, Mkuu wa mko huyo akizungumza na vyombo vya habari pamoja na wakazi wa hapo ameipongeza kampuni ya KC land kuweza kutekeleza sera ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha inatengeneza  mazingira bora ya uwekezaji  ya kutoa fursa   ya kufanya biashara  kwa sekta binafsi.

Vilevile Kunenge amewataka wakazi wa Ngoma Mapinduzi kutovamia maeneo yaliotengwa na  KC land kwa ajili yakujenga, Shule,Zahanati pamoja na nyumba za ibada.

“Niwaombe watendaji wa serikali  za mitaa tusiruhusu  sasa watu uvamia  kujenga hovyo hovyo maeneo yalioachwa wazi, sehemu ya zahanati ibaki kuwa ya zahanati na nyumba za ibada pamoja na shule  zibaki kuwa hivyo wazi.”Amesema RC Kunenge

Pia mkuu wa Mkoa huyo amewaahidi wakazi hao kuwa ataongea na talula  kwa ajili ya ujenzi wa barabara ili kuhakikisha miundo mbinu inazidi kufika katika halmashauri hiyo ya wilaya ya Kigambioni.

Kwa upande wake mwenyekiti wa KC land development plan Khalid Mwinyi amesema kuwa mradi huo umejikita katika kutoa huduma kukopesha viwanja safi viliokwisha pimwa  kwa mkopo wa muda mrefu usio na riba.

Mwenyekiti huyo  amesema kuwa umuhimu wa kuwa na ardhi iliopimwa, vilevile amesema wameona  wafanye pia utaratibu rafiki  kuhakikiasha wanachi  wanapata viwanja kwa bei nafuu ili kutimiza ndoto  zao maana anaamini  kila mtu anatamani kuwa na nymba bora ambapo mpaka sasa hekari 1500 zimesha gaiwa kwa wananchi  hao kati ya 1800.

Mbali na hilo mweyekiti huyo amesema kuwa pia wanatoa huduma ya  mikopo ya vifaa vya ujenzi  kwa wateja hao.

“Tunao mradi wa ujenzi shirikishi ambapo tunatoa  vifaa vya ujenzi ili kuwaondolea  wananchi wetu ugumu wa kununua vifaa hivyo.” A mesema Mwinyi.”

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge  akifanya zoezi la kuzindua kisima cha maji safi na salama ,ikiwa ni mradi uliofanywa na kampuni ya KC land development plan katika kijiji cha Ngoma Mapinduzi  halmashauri ya wilaya ya Kigamboni Jijini Dar es salaam,Akisaidiana na mwenyekiti mtendaji wa KC land Khalid Mwinyi.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge  akifungua bomba la maji katika uzinduzi huo wa kisima cha maji safi na salama  Ngoma Mapinduzi Jijini Dar es salaam.

Wakazi waNgoma Mapinduzi waliokusanyika  ambao tayari wana maeneo yao hapo, Jijini Dar es salaam.



from MICHUZI BLOG

No comments