Breaking News

Shughuli za uokozi zaendelea nchini Uturuki baada ya tetemeko la ardhi


Vikosi vya waokoaji vimeendelea na juhudi za kuwatafuta watu walioathirika na tetemeko la ardhi nchini Uturuki. Mpaka sasa watu 27 wameshakufa kutokana na tetemeko hilo lilitokea hapo jana. 

Tetemeko hilo lilikumba eneo la bahari linalojumuisha Uturuki na Ugiriki. Watu 25 wamekufa kwenye maneneo ya pwani ya Uturuki na vijana wawili wamekufa kwenye kisiwa cha Ugiriki cha Samos. Watu wengine zaidi ya 800 wamejeruhiwa nchini Uturuki.

 Na kwa mujibu wa taarifa majengo yapatayo 20 yameteketezwa katika mji wa Izmir wa nchi hiyo. Mitetemeko mingine zaidi ya 400 ilifuatia. 

Viongozi wa Uturuki na Ugiriki wamewasiliana kwa njia ya simu kuzungumzia juu ya maafa hayo.



from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/2TEiEQ6

No comments