Breaking News

Marekani: Donald Trump na Joe Biden wafanya kampeni za mwisho


Rais Donald Trump na mshindani wake,Joe Biden wamo katika hatua za mwisho za kampeni zao za uchaguzi wa rais utakaofanyika tarehe tatu ya mwezi ujao.

 Rais wa hapo awali Barack Obama atauungana na mgombea huyo wa chama cha Demokratic Joe Biden kufanya kampeni kwenye jimbo la Michigan wakati Donald Trump ataekeleza nguvu zake katika jimbo la Pennsylivania ambalo ni muhimu. 

Mgombea mwenzi wa Biden bibi Kamala Harris aliendeleza kampeni katika jimbo la Texas hapo jana Ijumaa ili kujaribu kuligeuza jimbo hilo liwe la chama cha Demokratic kwa mara ya kwanza tangu enzi za rais Jimmy Carter mnamo mwaka 1976. 

Ikiwa mgombea wa chama cha Demokratic, Joe Biden atashinda kwenye jimbo hilo, rais Trump atapata pigo kubwa.



from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3kJqAeU

No comments