Ulinzi waimarishwa nchini Ufaransa baada ya mauaji kanisani
Serikali ya Ufaransa imeazimia kuwaweka maelfu ya polisi kulinda mitaa, wakati ambapo uchunguzi ukifanyika juu ya kijana aliyekuwa na nasaba ya Tunisia aliyewaua watu watatu ndani ya kanisa katika mji wa Nice, kusini mwa Ufaransa.
Kijana huyo, mwenye umri wa miaka 21 alipigwa risasi na polisi na kujeruhiwa. Aliwasili nchini Ufaransa mnamo mwezi huu kwa kupitia Italia kabla ya kufanya maauji hayo ambayo serikali ya Ufaransa imekitaja kitendo kuwa ni cha kigaidi na kilichosababishwa na itikadi kali.
Mtuhumiwa wa mauaji anayetambulika kwa jina la Brahim Issaou alipigwa risasi mara kadhaa na polisi mpaka kufikia jana Ijumaa alikuwa bado hajapata fahamu hospitalini.
Rais wa Urafansa Emmanuel Macron aliitisha kikao cha dharura juu ya kadhia hiyo ameshaimarisha doria za kijeshi kwenye makanisa na kwenye sehemu nyingine kabla ya siku kuu ya watakatifu hapo kesho Jumapili.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/3mFzCtU
No comments