Waziri Mkuu wa Libya al-Serraj aahirisha ajiuzulu
Waziri Mkuu wa Libya, Fayez Serraj, wa serikali inayotambuliwa kimataifa ameahirisha uamuzi wake wa kukabidhi madaraka mwishoni mwa Oktoba.
Serraj atasalia kuwa kiongozi wa taifa hilo hadi mazungumzo ya kisiasa yakamilike, ili kuepusha ombwe la kisiasa nchini humo. Awali alitangaza waziri mkuu huyo alitangaza kukabidhi madaraka kwa mamlaka ya utendaji mwishoni mwa mwezi huu wa Oktoba.
Msemaji wa Baraza la Juu la Uongozi Libya, Ghaleb Al-Zaqlaly, amesema matumaini yake ni kwamba kamati ya mazungumzo itawajibika na kuweka mbali masilahi ya kibinafsi, na ya kikanda, ili nchi hiyo iweze kumaliza mgogoro wa sasa kwa amani na maelewano.
Libya imetumbukia katika machafuko tangu kupinduliwa kwa dikteta Moamer Gaddafi mwaka 2011.
from MUUNGWANA BLOG https://ift.tt/35TUp6r
No comments