Breaking News

TANGAZENI MIRADI YA MAENDELEO - WAZIRI TABIA.


 

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Tabia Mwita


Na Mwandishi Wetu 

Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini wametakiwa kutangaza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya sita na namna ambavyo wananchi watanufaika kupitia uwepo wa miradi hiyo.

Hayo yamesemwa leo tarehe 30 Machi 2023 na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Tabia Mwita wakati akifunga kikao kazi cha 18 cha Maafisa habari hao kinachofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa  Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam

“Eneo hili la miradi ya maendeleo ni pana na linagusa maisha ya wananchi, hivyo Maafisa Mawasiliano wote mlioko hapa pasipo kujali umetoka kwenye Taasisi au Wizara kazi zenu zinagusa wananchi hivyo tunawategemea ninyi katika utoa taarifa zinazolenga kuhamasisha ushiriki wao katika programu mbalimbali za maendeleo nchini na kujenga taswira chanya ya Serikali yetu kwa wananchi wetu” amesema Waziri Tabia.

Katika upande mwingine, Waziri Tabia amewataka Maafisa habari hao kuelekeza nguvu zao katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa sababu unamgusa kila mwananchi.

“Wote tunafahamu ifikapo mwaka 2024 tuna zoezi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo Majukumu ya Serikali za Mitaa ni Kuwezesha na kudumisha utulivu, amani na utawala bora, Kudumisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii na miundo mbinu, kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii na Kulinda mazingira kwa lengo la kuchangia katika maendeleo endelevu,” ameeleza Waziri Tabia.






No comments